Imeandikwa na:
Ummu Nassra
Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua, na wanaichukulia ni maskhara. Hao watapata adhabu ya kuwafedhehesha Maulamaa pamoja na wafasiri wengi wa Quraan wameeleza kuwa neno "Lahwal-hadith" katika aya hii inakusudiwa nyimbo na zana za miziki.
Mfano Ibn Mas'uud Radhiya Allahu 'anhu amesema kuhusu Aya hii "Naapa kwa Allah hii inamaanisha ni nyimbo" Pia miongoni mwa hadithi zenye kuonyesha uharamu wa ngoma na kila aina ya muziki ni hadithi mashuhuri ya Mtume Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam:
"Watakuweko watu katika Ummah wangu watakaojaribu kuhalilisha zinaa, uvaaji wa hariri, pombe na muziki. Bukhari
Ni vyema tuelewe kuwa hakuna chochote alichokikataza Allah Subhaanahu wa Taala isipokuwa kina madhara ndani yake katika ustawi wa jamii. Jua kuwa miziki tunayoichezesha majumbani yanaweza kuchochea hisia za mja, jazba pamoja na muengezeko wa mapigo ya moyo na kushughulisha akili.
Ujumbe unaopatikana katika miziki na nyimbo nyingi hasa wakati huu tulionao huenda kinyume kabisa na maadili ya Kiislamu, huamsha hisia za mapenzi, uzinzi na uhuru wa kufanya lolote bila ya kuzingatia wajibu wa mja. Umefika wakati kwa Waislamu kutanabahi na kujaribu kwa kadiri ya uwezo wetu kuepukana na balaa hili na kurejesha mandhari nzuri ndani ya majumba yetu. Tusiziuwe nyumba zetu kwa sauti za shetani (nyimbo na miziki) na kuwawekea makaazi, Ni lazima tuziuhishe nyumba zetu kuwa ni sehemu ya kumkumbukwa Allah Subhaanahu wa Taala (dhikr) kwa kila hali; kwa sala, kusoma Quraan, na vitabu vyengine vya dini pamoja na masuala mbali mbali yanayowahusu Waislamu. Hii itatupelekea kuzungukwa na Malaika, kulindwa na kupata ridhaa ya Allah Subhaanahu wa Taala.
MCHANGANYIKO WA WANAUME NA WANAWAKE
Moja katika jambo linaloonekana ni la kawaida hasa katika majumba yetu ni michanganyiko ya wanaume na wanawake (Ikhtilaatw). Ni wajibu wa kila Muislamu kuelewa hukumu ya kisheria juu ya jambo hili. Ikhtilaatw ni kuchanganyika kwa wanawake na wanaume waliokuwa sio maharim ima kwa wingi au uchache katika sehemu moja. Hali hii imezoeleka sana majumbani mwetu, katika shughuli zetu zikiwa ni za furaha au misiba au hata siku za kawaida.
Tuelewe kuwa mijumuiko ya aina hii na kudhihirika mapambo ni kitu kilichokatazwa katika sheria kwa sababu huwa ni mzizi wa fitina na ni kichochezi cha maasia mengine kwani shaytwan huwa pamoja nao. Katika hadithi iliyosimuliwa na 'Umar, Radhiya Llahu 'Anhu inatueleza:
Kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Hachanganyiki mwanamume na mwanamke ila shaytwaan huwa ni watatu wao. [At-Tirmidhiy]
Dini yetu imetuwekea adabu maalum; na kama kuna ulazima wa kuchanganyika majumbani, basi ni vyema kuwe na sehemu tofauti kati ya wanaume na wanawake pindi wakikujia kwao. Tunatakiwa tuwe na hadhari tunapotembelewa na mgeni, hata kama ni ndugu wa mume au mke. Mtume Swalla Llahu 'Alayhi wa Ssalaam aliwaeleza maswahaba zake na Waislamu wote kuwa: Tahadharini kuingilia majumbani mwao wanawake; Wakasema: Ewe Mjumbe wa Allaah, je, vipi kuhusu shemeji? Akasema: Shemeji ni mauti Al-Bukhaariy na Muslim]
Pia Allaah Subhanahu wa Taala anatueleza katika Suuratul Al-Ahzaab: 53
Nanyi mnapowauliza (wakeze) waulizeni nyuma ya pazia. Kufanya hivyo kunasafisha nyoyo zenu za zao. Ni jukumu letu kama ni wazazi kuzielewa sheria hizi na kuzidi kuzipamba nyumba zetu katika mandhari nzuri ya kiislam. Hii itasaidia hata na vizazi vyetu kuinukia kwa maadili na tabia njema na kujua mipaka yao. Na kama itatokea kwa mwanamme au mwanamke kutembea au kutembelewa na kukutana na mwenyeji wa jinsia tofauti basi na tumuogope Allaah na kujihifadhi kwa kadiri ya uwezo wetu, bila ya kurefusha mazungumzo.
Allaah Alietukuka Anatufahamisha katika Suuratu Nnuur:30-31
Wambie waumini wanaume wainamishe macho yao (wasitazame yaliyokatazwa) na wazilinde tupu zao hili ni takaso kwao; bila ya shaka Allaah anazo habari za wanayoyafanya. Na wambie waumini wanawake wainamishe macho yao na wazilinde tupu zao, wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika.
BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM
UTANGULIZI
Hakika shukrani zote ni zake Allaah Subhaanahu Wata’ala, tunaemshukuru, tunaemtegemea, kumtaka msamaha na kutubu kwake. Tunajikinga Kwake Allaah Subhaanahu Wata’ala kutokana na shari za nafsi zetu na makosa ya matendo yake. Mwenye kuongolewa na Allaah hakuna wa kumpotoa, na mwenye kumpotoa hakuna wa kumuongoa. Rehma na Amani ziwe juu ya kipenzi chetu Muhammad SwallaAllahu ‘Alayhi wa Aalihi wa Sallam.
‘Amma Ba’ad
Nyumba ni neema kubwa ambayo mwanadamu amebarikiwa, [An-Nahl 16:80]
وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّنۢ بُيُوتِڪُمۡ سَكَنً۬ا
Na MwenyeziMungu amekujaalieni majumba yenu yawe maakaazi (yenu)
Kuweka mazingira sahihi ndani ya majumba ni jukumu la kila muislam mume na mke, na ni lazima mazingira hayo yaoane sambamba na sheria alizotuwekea Allah Subhanahu wa Ta’ala. Moja kati ya njia ya kuyafikia hayo ni kuepukana na kila aina ya uovu na uharibifu ndani ya majumba.
Kuna sababu nyingi kwa mwenye kuamini kuwa makini katika kuijenga na kuilinda nyumba yake katika misingi mema ya kiislam. Miongoni mwa sababu hizo ni:
1. Kujilinda yeye pamoja na familia yake kutokana na moto wa jahannam, na kujiweka mbali na ghadhabu zake. [At-Tahriym 66:6]
يَـٰٓأَيُّہَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ قُوٓاْ أَنفُسَكُمۡ وَأَهۡلِيكُمۡ نَارً۬ا وَقُودُهَا ٱلنَّاسُ وَٱلۡحِجَارَةُ
Enyi mlioamini! Jiokoeni nafsi zenu na watu wenu na moto ambao ambao kuni zake ni watu na mawe.
2. Kujua wajibu wake juu ya jukumu la kuchunga nyumba, na kujiweka tayari kujibu kwa kila unachokichunga. Hadith:
Kutoka kwa Abdullah, Allah amuwie radhi, kwamba Mtume SwallaAllahu ‘Alayhu wa Aalihi wa Ssallam amesema:
“Nyote ni wachunga na nyote mtaulizwa juu ya mlivyovichunga. Kiongozi anaewaongoza watu ni mchunga na ataulizwa juu wachungwa wake. Mwanamume ni mchunga kwa watu wake wa nyumbani na ataulizwa juu ya wachungwa wake. Na mwanamke ni mchunga kwa nyumba ya mumewe na watoto wake nae ataulizwa juu ya wachungwa wake .Mtumwa ni mchunga katika mali ya bwana wake na anawajibika juu ya mali hiyo. Hakika nyote ni wachunga na na kila mmoja wenu anawajibika juu ya wachungwa wake”
Imesimuliwa na Bukhari na Muslim
3. Nyumba ni sehemu ya hifadhi kwa binaadamu, kujiweka mbali na kila aina ya ubaya na uovu ukiwa wa mnyama, binaadamu au majini, na kupata utulivu ndani yake. Amesema Mtume SwallaAllahu ‘Alayhu wa Ssallam:
Usalama wa mtu katika wakati wa fitnah ni kubakia nyumbani kwake.
Kilicho muhimu zaidi ni kuzingatia kuwa nyumba ni sehemu nyeti (muhimu) ya kujenga mazingira mazuri ya kiislam, kwani jamii bora hujengeka kuanzia nyumbani. Kwa masikitiko makubwa majumba yetu mengi yamejiweka mbali na mafundisho sahihi ya kiislam.
InshaAllaah katika makala hizi tutaweza kugusia na kutanabahisha baadhi ya vitu ambavyo huchangia kwa kiasi kikubwa kuharibika mfumo wa kiislam ndani ya majumba na jamii kwa ujumla, na kujaribu kutafuta njia muafaka kurejesha mazingira mazuri ndani ya majumba yetu.
Kuna mambo mengi ya wazi kabisa ambayo sheria yameyakataza katika Uislamu na jamii imeghafilika nayo. Mambo hayo huchangia kuharibika na kuhatarisha mfumo mzima wa kiislam ndani ya majumba. Miongoni mwa yenye kuhatarisha ni haya yafuatayo:
TELEVISHENI (TV) - LUNINGA.
Televisheni kama inavyojuilikana (TV) ni chombo ambacho hakikosekani katika kila nyumba. Kama kitatumika vizuri chombo hicho kwa mambo ya kheri yenye kuzidisha imani, kupeleka dini mbele, kukuweka mbali na maasi na kuhifadhi dini ya mja kinaweza kuleta faida. Na kama kitatumika vibaya kinaweza kuathiri familia kwa asilimia kubwa kabisa.
Ukweli ni kuwa kuangalia TV kuna madhara mengi na makubwa kuliko faida. Familia za kiislam zinaogelea kwa kasi kubwa bila ya kujali au kuona mabaya ya chombo hicho.
Tuchukue mfano mdogo tu wa athari za televisheni kwa watoto kama utafiti huu mdogo uliofanyika hapa Uingereza unavyofafanua.
Watoto wenye kuangalia televisheni kwa zaidi ya masaa mawili kila siku wanakabiliwa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa athma. Uchunguzi huo umeonyesha kuwa, kuangalia televisheni kwa muda mrefu kunaleta uwezekano wa kupata athma uongezeke mara mbili kwa watoto.
Jinsi mfumo wa kupumua unavyofanya kazi wakati mtoto anapokaa tu bila kufanya chochote, hupelekea kutokea mabadiliko katika mapafu pamoja na magojwa mengine ya kupumua ikiwemo athma.
Unene wa kupita kiasi pamoja na kutokufanya mazoezi kunakosababishwa na kuangalia muda mrefu televisheni hupelekwa kutokea hali hiyo Wataalamu wamesema kuwa, kuishi maisha ya kutokuwa na harakati yoyote katika umri mdogo hupelekea kuongezeka uwezekano wa hatari ya kupata athma ukubwani.
Hivyo wamewashauri wazazi kuwashajiisha watoto wao kufuata maisha ya kawaida ya kuwa na mishughuliko na kupunguza muda wanaoutumia kuangalia TV.
Wataalamu wa Uingereza wametoa taarifa hiyo baada ya kuwafanyia uchunguzi watoto 3,000 kuanzia wale waliozaliwa mpaka walio na miaka 11.
Hasara moja ya kupoteza
muda kuangalia TV inaweza kuzaa makosa mengi ndani yake. Kuona na kusikiliza
kunawavutia wengi na kuwafanya watu kutawaliwa na tabia hiyo na kutoweza
kuiepuka. Hakuna shaka kuwa jamii hasa watoto imeathirika sana na jambo hili.
TV inasababisha kwa kiasi kikubwa watoto wa Kiislamu kutumbukia katika tabia
zisizo na maadili, ulevi, uzinzi, kukosa heshima, kujinasibisha na uzungu na
mengi mengine maovu tunayoyaona katika jamii zetu. Yote hayo wanayaona na
kujifunza moja kwa moja kutoka kwenye TV.
Mtu huhisi kuwa anapoteza wakati tu kujistarehesha na TV, anayakata masaa na dakika kwa ajili ya chombo hicho, ni makosa!!. TV si chombo cha starehe, bali ni chombo kinachotumika kuchochea hisia, kubadilisha muelekeo na utiifu wa mtu. Na ndiyo hali halisi ndugu yangu Muislamu kama bado hujatanabahi.
Yafaa Waislamu tuzinduke na kuziona faida chache na hasara nyingi za chombo hiki. Kama tunaona ni neema hakika tutakuja kuulizwa namna tulivyoitumia. [At-Takaathur 102:8]
ثُمَّ لَتُسۡـَٔلُنَّ يَوۡمَٮِٕذٍ عَنِ ٱلنَّعِيمِ
Kisha mtaulizwa siku hiyo juu ya neema mlizopewa mlizitumiaje.
Na kwa hakika hata masikio na macho tunayoyatumia kwa chombo hicho pia tutakuwa ni wenye kuulizwa. Hivyo ni juu yetu kuchagua ni kipi cha kutizama. [Al-Israa 17:36].
إِنَّ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡبَصَرَ وَٱلۡفُؤَادَ كُلُّ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ كَانَ عَنۡهُ مَسۡـُٔولاً
Hakika masikio na macho na moyo, hivyo vyote vitaulizwa
Tv ni kama upanga ukiutumia vizuri unaweza kuleta faida na ukiitumia vibaya unaweza kuleta madhara makubwa. Kwa mfano mtu akiweza kuidhibiti na kuangalia kwa nadra kwa vipindi vya kheri vyenye kwenda sambamba na dini yetu inaweza kukubalika, bali ni wachache wenye kufanya hivyo. Wengi wao wameogolea na kuangalia tu bila hata ya kujali faida na hasara zake, na hii ndio iliopelekea madhara kuwa mengi kuliko faida.
Miongoni mwa madhara ya TV ni:
- Kunapoteza wakati bure na kupuuza mengi ya wajibu
- Inaeneza tamaduni za kikafiri kama ni njia moja ya kuigwa katika maisha
- Inaeneza upotofu na uhuru kwa kupitia katika michezo, nyimbo matangazo yasiyo ya heshima ambayo hupelekea watizamaji kutumbuka na tabia hizo za kijinga.
- Mazoea ya kuangalia TV yanaharibu akili na kuathiri afya ya mja.
Hivyo kama kuna watu wazuri wenye kumuogopa Allah Subhaanahu Wata’ala na kuonyesha mazuri yenye faida bila ya kukiuka mipaka ya Allah, basi unaweza kuangalia na ni jambo la kupendeza kwa wengi. Ni vyema kuchunga aina gani ya vipindi tunavyoangalia ndani ya majumba yetu.
Ni wajibu wa kila mtu kueleweka wazi madhara na faida ya kifaa hichi ili tuweze kukitumia vyema ama kujiepusha nacho kabisa ikiwa tutashindwa kuweka vidhibiti katika majumba jinsi chombo hiki kitumike katika kunufaisha, kuelimisha na kuleta faida na si kuharibu, kupoteza muda na kupelekea jamii iliyozugika na hatimaye kupotoka na kupotosha wengine.
UVUTAJI SIGARA
Uvutaji wa sigara umeenea na kushamiri dunia nzima licha ya kuwa madhara yake yapo wazi. Baadhi ya Waislamu wametumbukia katika balaa hili na kuziathiri nyumba zao bila ya kujijua. Kuna sababu tosha zenye kuonyesha uharamu wa jambo hili kwa Muislamu. Sigara ina athari sana katika dini, afya, mazingira, familia, rasilimali na mengineyo.
i. MADHARA KATIKA DINI
Sigara inaathiri ibada ya mja na inapunguza malipo ya ibada hiyo. Kwa mfano ibada ya sala ambayo ni nguzo muhimu ya Muislamu; Kutokana na hadithi iliyosimuliwa na wengi; Amesema Mtume Swalla Llahu Alayhi wa Ssalam
“Mwenye kula Kitungu maji au thawm, basi asiukaribie Msikiti wetu na akae nyumbani”
[Bukhari na Muslim]
Tunaona makatazo yamekuja kutokana na harufu mbaya inayotokana na vitu hivyo amabayo huwakirihisha watu pamoja na Malaika katika nyumba za Allaah (Misikitini).
Bila ya shaka mdomo wa mvutaji sigara una harufu mbaya zaidi kuliko vitunguu, ima huwakera watu na Malaika kwa harufu hiyo au kukosa fadhila za sala ya jamaa msikitini kwa mwanamme.
i. MADHARA KATIKA MWILI
Hakuna anaepinga madhara ya sigara katika mwili wa binadam. Utafiti wa kiafya umeyaona haya na kuyaeleza kwa kina; hata imekuwa ni sheria kuweka wazi maandishi ya tahadhari kwa kila paketi la sigara angalau watu wazinduke.
Ndani ya sigara hupatikana kemikali zenye sumu kama vile nicotine, arsenic, carbon monoxide na vyenginevyo ambavyo mvutaji huathirika kidogo kidogo hadi kuua sehemu muhimu za mwili wake. Athari za zake ni kubwa na ni nyingi; husababisha cancer, TB, mshituko wa moyo, pumu, ubovu wa meno, na huwa ni chimbuko la maradhi mengi mengineyo.
Allaah Alietukuka anatuonya tusiwe wenyenye kujidhuru. Suuratu Nnisaa’:29
وَلَا تَقۡتُلُوٓاْ أَنفُسَكُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِكُمۡ رَحِيمً۬ا
Wala msijiue, hakika Allah ni mwenye kukurehemuni
Pia katika Suuratul Baqarah:195
وَلَا تُلۡقُواْ بِأَيۡدِيكُمۡ إِلَى ٱلتَّہۡلُكَةِ
Wala msjiitie kwa mikono yenu katika maangamizo
Na Mtume Swalla Allahu ‘Alayhi Wasallam anasema katika Hadithi:
" لا ضرر ولا ضرار "
Kusiwe na kudhuriana wala kulipa dhara.
ii. ATHARI KWA AKILI NA MATAMANIO
Sigara huathiri akili ya mwanadamu kwa kiasi kikubwa. Mvutaji mzoefu anapoikosa huwa vigumu kwake kufikiri kitu, kutatua tatizo au kuwa makini katika jambo mpaka aipate. Badala kuwa mtumwa wa Mola wake, hugeuka na kuwa mateka wa sigara yake na kuifanya dhaifu akili na hisia zake.
Allah Subhaanahu wa Ta’ala anatueleza katika Suuratu An-Nisaa’:27
وَٱللَّهُ يُرِيدُ أَن يَتُوبَ عَلَيۡڪُمۡ وَيُرِيدُ ٱلَّذِينَ يَتَّبِعُونَ ٱلشَّہَوَٲتِ أَن تَمِيلُواْ مَيۡلاً عَظِيمً۬ا
Allah anataka kukukhafifishieni. Lakini wanaofuata matamanio yao wanataka mkengeuke mkengeuko mkubwa
iii. MADHARA KATIKA MALI
Mvutaji sigara hupoteza pesa nyingi karibu kila siku kununulia sigara isiyomletea tija yeyote bali ni kuwafaidisha hao wanaoendesha bishara hii haramu. Kumbuka kuwa mali tunayoipata tutakuja kuulizwa kwa njia gani tumeichuma na vipi tumeitumia.
Katika Suurat An-nisaa’:5 Allah Subhaanahu Wata’ala anatueleza:
وَلَا تُؤۡتُواْ ٱلسُّفَهَآءَ أَمۡوَٲلَكُمُ ٱلَّتِى جَعَلَ ٱللَّهُ لَكُمۡ قِيَـٰمً۬ا وَٱرۡزُقُوهُمۡ فِيہَا
Wala msiwape wapumbavu mali zenu ambazo Allah amezijaalia kwa maisha yenu
Pia katika Suuratul Israa:26 – 27
وَلَا تُبَذِّرۡ تَبۡذِيرًا إِنَّ ٱلۡمُبَذِّرِينَ كَانُوٓاْ إِخۡوَٲنَ ٱلشَّيَـٰطِينِۖ
Wala usitawanye (mali yako) kwa ubadhirifu. Hakika watumiao kwa ubadhirifu ni ndugu wa mashetani
Na kutoka kwa Mtume Swalla Allahu ‘Alayhi Wasallam anasema:
" إن الله ينهاكم عن قيل وقال ، وكثرة السؤال وإضاعة المال
Hakika Allah anakukatazeni na mazungumzo yasiyokuwa na faida (huyu kasema au kimesemwa) na kukithirisha kuuliza masuali na kupoteza mali.
Licha ya nchi za Magharibi kutoa indhaari tu katika paketi kuonesha madhara ya sigara, Maulamaa wa kiislamu takriban wote wamekubaliana kwamba sigara ni haraam. Angalia Fatwa ifuatayo kutoka katika Fataawa Islaamiyah 442/3
Kuvuta sigara ni haraam kwa sababu ya kuleta madhara mengi wakati Allah Subhaanahu Wata’ala amehalalisha kwa waja wake vyote vilivyo vizuri katika vyakula na vinywa na akaharamisha vibaya vyao. Na aina zote za uvutaji ni miongoni mwa vitu vibaya kwa sababu ya kuleta madhara na kulewesha.
Ni vyema kutanabahi ndugu Muislamu na kuachana na mazoea sugu na potofu ya kuvuta sigara. Mvutaji sigara huwa hajali kuvuta mbele ya wale waliomzunguka ndani ya nyumba yake, kama mkewe/mumewe, watoto na wengineo. Huwasababishia kuvuta moshi wa sumu na wale walio karibu nae. Huleta hali mbaya hasa kwa mazingira ya ndani ya nyumba na ni mfano mbaya kwa kile kinachochungwa (mke na watoto) ndani ya nyumba hiyo.
Ndugu yangu Muislamu , kama ni miongoni mwa wenye kuendeleza uovu huu basi rudi kwa Mola wako kwa moyo ulio mwepesi wenye kusikiliza nasaha na kukubali yale yote yanayotoka kwa Mola kwa ajili ya kuinusuru nafsi yako kwanza, kisha dini yako, kisha akili yako, kisha familia yako, kisha mali yako na kadhalika.
MUZIKI NA NYIMBO
Miongoni mwa yenye kuzoeleka katika majumba yetu ni mziki. Kwa kweli
mziki umeenea kila pembe ya dunia kiasi ambacho unawaumiza Waislamu
wengi kimwili na kiakili bila ya kujijua. Kila mtu amekabiliana na hali
ambayo humuingiza kusikiliza muziki ama kwa hiari au kwa lazima.
Kuongezeka umaarufu wa muziki kunahatarisha sana majumba ya Waislamu na
hatimae kutumbukia katika balaa hilo usiku na mchana
Ukweli ni kuwa muziki unaathiri sana mioyo ya Waislamu na kuishughulisha
akili kwa mambo ya kipuuzi. Tunatumia muda na pesa nyingi katika
kununulia CD za majimbo yasiyo na faida, zana za miziki, na hata
kuwatumbukiza watoto wetu kwa vifaa (toys) mbali mbali vilivyojaa
miziki; Tunajitia makosani na kuuporomoa itikadi sahihi ya Muislamu.
Kuna dalili tosha katika Quraan na Sunnah zenye kuonyesha uharamu wa
muziki. Katika Suurat Luqmaan aya ya 6 Allaah Subhaanahu wa Ta'ala
anatueleza:
((وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْتَرِي لَهْوَ الْحَدِيثِ
لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ اللَّهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًا
أُولَئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ))
Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua, na wanaichukulia ni maskhara. Hao watapata adhabu ya kuwafedhehesha Maulamaa pamoja na wafasiri wengi wa Quraan wameeleza kuwa neno "Lahwal-hadith" katika aya hii inakusudiwa nyimbo na zana za miziki.
Mfano Ibn Mas'uud Radhiya Allahu 'anhu amesema kuhusu Aya hii "Naapa kwa Allah hii inamaanisha ni nyimbo" Pia miongoni mwa hadithi zenye kuonyesha uharamu wa ngoma na kila aina ya muziki ni hadithi mashuhuri ya Mtume Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam:
"Watakuweko watu katika Ummah wangu watakaojaribu kuhalilisha zinaa, uvaaji wa hariri, pombe na muziki. Bukhari
Ni vyema tuelewe kuwa hakuna chochote alichokikataza Allah Subhaanahu wa Taala isipokuwa kina madhara ndani yake katika ustawi wa jamii. Jua kuwa miziki tunayoichezesha majumbani yanaweza kuchochea hisia za mja, jazba pamoja na muengezeko wa mapigo ya moyo na kushughulisha akili.
Ujumbe unaopatikana katika miziki na nyimbo nyingi hasa wakati huu tulionao huenda kinyume kabisa na maadili ya Kiislamu, huamsha hisia za mapenzi, uzinzi na uhuru wa kufanya lolote bila ya kuzingatia wajibu wa mja. Umefika wakati kwa Waislamu kutanabahi na kujaribu kwa kadiri ya uwezo wetu kuepukana na balaa hili na kurejesha mandhari nzuri ndani ya majumba yetu. Tusiziuwe nyumba zetu kwa sauti za shetani (nyimbo na miziki) na kuwawekea makaazi, Ni lazima tuziuhishe nyumba zetu kuwa ni sehemu ya kumkumbukwa Allah Subhaanahu wa Taala (dhikr) kwa kila hali; kwa sala, kusoma Quraan, na vitabu vyengine vya dini pamoja na masuala mbali mbali yanayowahusu Waislamu. Hii itatupelekea kuzungukwa na Malaika, kulindwa na kupata ridhaa ya Allah Subhaanahu wa Taala.
MCHANGANYIKO WA WANAUME NA WANAWAKE
Moja katika jambo linaloonekana ni la kawaida hasa katika majumba yetu ni michanganyiko ya wanaume na wanawake (Ikhtilaatw). Ni wajibu wa kila Muislamu kuelewa hukumu ya kisheria juu ya jambo hili. Ikhtilaatw ni kuchanganyika kwa wanawake na wanaume waliokuwa sio maharim ima kwa wingi au uchache katika sehemu moja. Hali hii imezoeleka sana majumbani mwetu, katika shughuli zetu zikiwa ni za furaha au misiba au hata siku za kawaida.
Tuelewe kuwa mijumuiko ya aina hii na kudhihirika mapambo ni kitu kilichokatazwa katika sheria kwa sababu huwa ni mzizi wa fitina na ni kichochezi cha maasia mengine kwani shaytwan huwa pamoja nao. Katika hadithi iliyosimuliwa na 'Umar, Radhiya Llahu 'Anhu inatueleza:
Kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Hachanganyiki mwanamume na mwanamke ila shaytwaan huwa ni watatu wao. [At-Tirmidhiy]
Dini yetu imetuwekea adabu maalum; na kama kuna ulazima wa kuchanganyika majumbani, basi ni vyema kuwe na sehemu tofauti kati ya wanaume na wanawake pindi wakikujia kwao. Tunatakiwa tuwe na hadhari tunapotembelewa na mgeni, hata kama ni ndugu wa mume au mke. Mtume Swalla Llahu 'Alayhi wa Ssalaam aliwaeleza maswahaba zake na Waislamu wote kuwa: Tahadharini kuingilia majumbani mwao wanawake; Wakasema: Ewe Mjumbe wa Allaah, je, vipi kuhusu shemeji? Akasema: Shemeji ni mauti Al-Bukhaariy na Muslim]
Pia Allaah Subhanahu wa Taala anatueleza katika Suuratul Al-Ahzaab: 53
Nanyi mnapowauliza (wakeze) waulizeni nyuma ya pazia. Kufanya hivyo kunasafisha nyoyo zenu za zao. Ni jukumu letu kama ni wazazi kuzielewa sheria hizi na kuzidi kuzipamba nyumba zetu katika mandhari nzuri ya kiislam. Hii itasaidia hata na vizazi vyetu kuinukia kwa maadili na tabia njema na kujua mipaka yao. Na kama itatokea kwa mwanamme au mwanamke kutembea au kutembelewa na kukutana na mwenyeji wa jinsia tofauti basi na tumuogope Allaah na kujihifadhi kwa kadiri ya uwezo wetu, bila ya kurefusha mazungumzo.
Allaah Alietukuka Anatufahamisha katika Suuratu Nnuur:30-31
Wambie waumini wanaume wainamishe macho yao (wasitazame yaliyokatazwa) na wazilinde tupu zao hili ni takaso kwao; bila ya shaka Allaah anazo habari za wanayoyafanya. Na wambie waumini wanawake wainamishe macho yao na wazilinde tupu zao, wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika.
No comments:
Post a Comment