Mwenyezi Mungu Anasema:
{{Na
ambao pindi wafanyapo uchafu au wakajidhulumu nafsi zao humkumbuka
Mwenyezi Mungu na wakamwomba msamaha kwa dhambi zao - na nani anaye futa
dhambi isipo kuwa Mwenyezi Mungu? - na wala hawaendelei na waliyo
yafanya na hali wanajua.}} [Al-‘Imraan: 135]
Imesimuliwa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mwenyezi
Mungu huifurahia toba ya mja wake kuliko mmoja wenu anapokuwa juu ya
mnyama wake jangwani akamuangusha na kumkimbia.)) [Imepokewa na Al-Bukhaariy]
Na katika riwaya ya Muslim na wengine:
((Mwenyezi
Mungu huifurahia toba ya mja wake kuliko mmoja wenu anapokuwa juu ya
mnyama wake jangwani akamuangusha na kumkimbia. Mnyama huyo akiwa
amebeba chakula chake na maji yake, kisha mtu huyo akakata tamaa,
akauendea mti na kuegemea chini ya kivuli chake akiwa keshakata tamaa ya
kumuona mnyama wake tena. Na anapokuwa katika hali hiyo, ghafla
anamuona mnyama wake mbele yake. Akazishika hatamu zake, kisha akasema
kwa furaha: "Mola wangu Wewe ni mja wangu na mimi ni mola wako".
Alikosea kwa wingi wa furaha.))
Na maana ya Mwenyezi Mungu kuifurahia toba hiyo ni kuwa anaridhika na nia ya mja wake huyo juu ya kuwa alikosea kutamka.
Miongoni mwa du’aa za kuomba maghfira, ni hii du’aa inayoitwa 'Sayyidul-Istighfaar' (Du’aa
bora ya kuomba maghfira kupita zote) aliyotuusia Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Du’aa ambayo ndani
yake imekusanya maana zote za tawbah na kukiri, na kwamba hapana mwenye
kusamehe makosa isipokuwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala).
Imeposimuliwa kutoka kwa Shaddaad bin ‘Aws (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Bwana wa kuomba maghfira ni kusema:
اللَّهُمَّ
أَنْتَ رَبِّي لا إِلَهَ إلا أَنْتَ خَلَقْتَنِي وَأَنَا عَبْدُكَ وَأَنَا
عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا
صَنَعْتُ أَبُوءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ وَأَبُوءُ لَكَ بِذَنْبِي
فَاغْفِرْ لِي فَإِنَّهُ لا يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلا أَنْتَ.
Allaahumma
anta Rabbiy laa ilaaha illa Anta. Khalaqtaniy wa ana ‘abduka. Wa ana
‘alaa ‘ahadika wa wa’adika ma statwa’atu. A’udhu bika min sharri ma
swana’atu. Abu-u laka bini’imatika ‘alayya wa abu-u laka bidhanbiy,
faghfirliy, fainnahu laa yaghfiru dhunuuba illaa anta.
Akasema: Atakayesema
hayo wakati wa mchana akiwa na yakini juu yake akafa siku hiyo kabla ya
usiku kuingia, huyo ni katika watu wa Peponi. Na atakayesema hayo
wakati wa usiku akiwa na yakini juu yake akafa kabla ya asubuhi kuingia,
huyo ni katika watu wa Peponi.)) [Imepokewa na Al-Bukhaariy, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na wengine]
Maana Yake
Ee Allaah. Wewe ni Mola wangu hapana anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Wewe
|
اللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّي لا إِلَهَ إلا أَنْتَ
|
Umeniumba na mimi ni mja Wako
|
خَلَقْتَنِي وَأَنَا عَبْدُكَ
|
Na mimi nimo katika kutekeleza maamrisho Yako na waadi Wako niwezavyo
|
وَأَنَا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ
|
Ninajikinga Kwako na kila shari niliyoitenda
|
أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ
|
Ninakiri Kwako kwa neema Zako juu yangu
|
أَبُوءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ
|
Na ninakiri Kwako juu ya dhambi zangu
|
وَأَبُوءُ لَكَ بِذَنْبِي
|
Kwa hivyo unisamehe kwa sababu hapana mwenye kusamehe madhambi isipokuwa Wewe
|
فَاغْفِرْ لِي فَإِنَّهُ لا يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلا أَنْتَ.
|
No comments:
Post a Comment