Tuesday, 17 May 2016
Tuesday, 20 October 2015
Fadhila Za Mwezi Wa Muharram
Imeandikwa na Alhidaaya
AlhamduliLLaah, Tunamshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Kutufikisha tena katika mwaka mwengine mpya wa Kiislamu. Katika mwezi wa Muharram, kuna fadhila zake maalumu juu ya kwamba ni sawa na miezi mitukufu mingineyo. Fadhila nyingi Muislamu anaweza kuzipata atakapotekeleza maamrisho ili aweze kujichumia thawabu nyingi. Mojawapo ni funga ya tarehe 9 na 10 Muharram zinazojulikana kamaTaasu'aa na 'Aashuraa. Hivyo ndugu Waislamu tusiache kufunga siku hizi mbili kwani thawabu zake ni kama ilivyotajwa katika mapokezi yafuatayo:
قال النبي صلى الله عليه وسلم : (( صيام يوم عاشوراء ، إني أحتسب على الله أن يكفر السنة التي قبله)) رواه مسلم
Kasema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Funga ya siku ya 'Aashuraa, nataraji kutoka kwa Allaah Ayafute madhambi ya mwaka uliotangulia)) [Muslim]
(soma maelezo chini kujua kwanini tufunge pia na tarehe 9 Muharram)
Jumla ya miezi mitukufu ni minne na mwezi huu wa Muharram ndio mwezi wa kwanza unaoanza kuhesabika kama ni mwaka mpya.
((إِنَّ عِدَّةَ الشُّهُورِ عِندَ اللّهِ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا فِي كِتَابِ اللّهِ يَوْمَ خَلَقالسَّمَاوَات وَالأَرْضَ مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ذَلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ فَلاَ تَظْلِمُواْ فِيهِنَّأَنفُسَكُمْ))
((Idadi ya miezi (ya mwaka mmoja) mbele ya Allaah ni miezi kumi na mbili katika ilimu ya Allaah (Mwenyewe tangu) siku Alipoumba mbingu na ardhi. Katika hiyo imo minne iliyo mitukufu kabisa (nayo ni Rajab, Dhul-Qa'adah, Dhul-Hijjah na Muharram) (kufanya) hivi ndiyo dini iliyo sawa. Basi msijidhulumu nafsi zenu (kwa kufanya maasi) katika (miezi) hiyo)) [At-Tawbah 9:36]
Na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika Hadiyth iliyotoka kwa Abu Bakr (Radhiya Allaahu 'anhu):
(السنة اثنا عشر شهرا، منها أربعة حرم: ثلاث متواليات، ذو القعدة، وذو الحجة، والمحرم، ورجب مضر الذي بين جمادى وشعبان)) رواه البخاري، ومسلم
((Mwaka una miezi kumi na mbili, minne miongoni ya hiyo ni mitukufu, mitatu inafuatana pamoja; Dhul-Qa'adah, Dhul-Hijjah na Muharram na Rajab ambao uko baina ya (mwezi wa) Jumaada na Sha'abaan)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Ni neema kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Kutujuaalia kuwa na miezi iliyo bora kuliko miezi mingine au masiku bora au masaa bora kuliko mengine, ambazo thawabu za mema yanayotendeka humo huwa ni zaidi ya nyakati nyingine.
Kuhesabika Kwa Mwaka Mpya Wa Hijriyah
Miaka yetu ya Kiislam imeanza kuhesabika baada ya kuhama (Hijrah) kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba kutoka Makkah kuhamia Madiynah. Baada ya kuhama, 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) akatoa shauri kuwa kwa vile ni mara ya mwanzo wanahamia katika mji ambao wataanza kutumia Sharia'h ya Kiislam, basi ni bora kuanza kuhesabu miaka kwa kuanzia mwezi huo waliohama, nao ni mwezi uliojulikana kamaMuharram. Na pia inasemekana kuwa 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) alikuwa akipata barua kutoka kwa mabalozi wake wa nchi mbalimbali zilizokuwa chini ya Uislam, na zilikuwa zikiandikwa majina ya miezi bila tarehe. Akawashauri Maswahaba wenzake kuwa kuwe na tarehe. Wako waliopendekeza tarehe zianze kwa kufuata miaka ya kirumi, na wako waliopendekeza zianze kwa miaka ya kifursi. Mwishowe wakakubaliana ianze pale alipohamia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Madiynah.
Na mwaka huu wa Kiislam ambao unafupishwa kama A.H au H kwa kirefu yenye maana 'After Hijrah'au Hijriyah, tarehe 1 Muharram A.H ilikuwa ni sawa na tarehe 16 Julai 622M. Na ndivyo hivi inavyohesabika mpaka mwezi wa Dhul-Hijjah unapomalizika na mwezi wa Muharram utakapoingia hivi karibuni
Fadhila Za Mwezi Huu Khaswa
Ingawa miezi minne yote iliyotajwa katika Aayah ya juu ni mitukufu lakini mwezi huu wa Muharram umefadhilishwa zaidi ya miezi mingine kama ilivyo katika Hadiyth zifuatazo:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ((أَفْضَلُ الصِّيَامِ بَعْدَ رَمَضَانَ شَهْرُ اللَّهِ الْمُحَرَّمُ )) رواه مسلم
Imepokelewa na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kasema; Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Funga bora kabisa baada ya Ramadhaan ni funga ya mwezi wa Allaah wa Muharram)) [Muslim]
عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ : "مَا رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَتَحَرَّى صِيَامَ يَوْمٍ فَضَّلَهُ عَلَى غَيْرِهِ إِلّا هَذَا الْيَوْمَ يَوْمَ عَاشُورَاءَ وَهَذَا الشَّهْرَ يَعْنِي شَهْرَ رَمَضَنِان " رواه البخاري
Imepokelewa na Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) ambaye amesema: "Sijapata kumuona Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisubiri kufunga siku yoyotekama siku hii ya siku ya 'Aashuraa na mwezi huu yaani mwezi wa Ramadhaan" [Al-Bukhaariy]
Swawm ya 'Ashuraa imependezeshwa hata kwa watoto kuifunga kamawalivyokuwa wakifanya Maswahaba katika siku hiyo.
عن الرُّبيّع بنت معوذ رضي الله عنها قالت: "أرسل رسول الله صلى الله عليه وسلم غداة عاشوراء إلى قرى الأنصار "من أصبح مفطرا فليتم بقية يومه ومن أصبح صائما فليصم" ، قالت : فكنا نصومه بعد ونصوّمه صبياننا ... رواه البخاري ومسلم
Kutoka kwa Ar-Rubay'i bint Mu'awwadh (Radhiya Allaahu 'anhaa) amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituma ujumbe Alfajiri ya siku ya 'Ashuraa katika vijiji vya Answaar "Aliyeamka akiwa amefuturu amalize siku yake (kwa kutokula) na aliyeamka amefunga afunge" Akasema (Ar-Rubay'i: 'Tulikuwa tukifunga baada yake na tukiwafungisha watoto wetu...'[Al-Bukhaariy na Muslim]
Sababu Ya Kufunga Siku Ya 'Aashuraa
عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: " قَدِمَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمَدِينَةَ فَرَأَى الْيَهُودَ تَصُومُ يَوْمَ عَاشُورَاءَ فَقَالَ: ((مَا هَذَا)) قَالُوا هَذَا يَوْمٌ صَالِحٌ هَذَا يَوْمٌ نَجَّى اللَّهُ بَنِي إِسْرَائِيلَ مِنْ عَدُوِّهِمْ فَصَامَهُ مُوسَى، قَالَ: (( فَأَنَا أَحَقُّ بِمُوسَى مِنْكُمْ)) فَصَامَهُ وَأَمَرَ بِصِيَامِهِ" رواه البخاري
Imepokelewa na Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) kasema "Alielekea Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Madiynah akawaona Mayahudi wanafunga siku ya 'Aashuraa, akasema: ((Nini hii?)) (yaani kwa nini mnafunga?) Wakasema hii ni siku njema, hii ni siku Allaah Aliyowaokoa Wana wa Israili kutokana na adui wao, na Muusa alifunga siku hii. Akasema (Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mimi nina haki zaidi juu ya Muusa kuliko nyinyi)). Akafunga siku hiyo na akaamrisha ifungwe" [Al-Bukhaariy]
Lakini Mtume wetu (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametufundisha kuwa tukhitilafiane na Mayahudi kufunga siku hiyo kwa kuongeza siku moja kabla.
روى عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قال : "حِينَ صَامَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمَ عَاشُورَاءَ وَأَمَرَ بِصِيَامِهِ قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّهُ يَوْمٌ تُعَظِّمُهُ الْيَهُودُ وَالنَّصَارَى فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((فَإِذَا كَانَ الْعَامُ الْمُقْبِلُ إِنْ شَاءَ اللَّهُ صُمْنَا الْيَوْمَ التَّاسِعَ)) قَالَ فَلَمْ يَأْتِ الْعَامُ الْمُقْبِلُ حَتَّى تُوُفِّيَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّىاللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ". رواه مسلم
Imepokelewa na Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) kasema "Alipofunga Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) siku ya 'Aashuraa na akaamrisha ifungwe wakasema: Ewe Mtume wa Allaah, hii ni siku wanayoitukuza Mayahudi na Manaswara. Akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Ikifika mwakani In shaa Allaah tutafunga siku ya tisa pia)). Akasema (Ibn 'Abbaas) haukufika mwaka uliofuata ila alifariki Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)[Muslim]
Kwa hiyo ni bora kufunga siku ya tisa na kumi Muharram, na kama mtu hakujaaliwa kufunga siku ya tisa na kumi, basi afunge siku ya kumi peke yake ili asikose kupata fadhila ya siku hiyo.
Kwa vile siku hii ni siku Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Aliyomnusuru Muusa ('Alayhis-Salaam) na Wana wa Israaiyli, na sisi pia tutakaofunga tuwe na tegemeo kuwa nasi Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atatunusuru pia kutokana maadui wetu na mabaya kamaAlivyotuahidi In shaa Allaah
((إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ))
((Bila ya shaka Sisi Tunawanasuru Mitume Yetu na wale walioamini katika maisha ya dunia ya siku watakaposimama mashahidi (kushuhudia amali za viumbe)) [Ghaafir 40: 51]
Juu ya kwamba fadhila ya kufunga Swawm ni ibada Aipendayo kabisa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kamailivyo katika Hadiyth mbali mbali, vilevile funga hii itatusafisha na madhambi ya mwaka mzima,
قال النبي صلى الله عليه وسلم : (( صيام يوم عاشوراء ، إني أحتسب على الله أن يكفر السنة التي قبله))رواه مسلم
Kasema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Funga ya siku ya 'Aashuraa, nataraji kutoka kwa Allaah Ayafute madhambi ya mwaka wa nyuma)) [Muslim]
Ndugu Waislam, hii ni fursa kubwa ya kujisafisha na dhambi na kuzidisha taqwa (ucha Mungu) ili kujibebea zawadi nyingi twende nazo Akhera kwa vile hatujui amali njema zipi zitakazokubaliwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na hatujijui kama tutakuwa na umri wa kuchuma zaidi.
Bid'ah Katika Siku Ya 'Aashuraa
Katika mwezi huu wa Muharram, tarehe kumi ambayo ni siku ya 'Ashuraa, tunawaona baadhi ya watu wakifanya maandamano na kuvaa nguo nyeusi wakidai ni nguo za msiba, na huku wakijipiga vifua kwa ngumi na wengine kujikata kwa visu, kujipiga kwa minyororo na damu kuwamwagika, wakidai wanaomboleza kifo cha mjukuu wa Mtume, Al-Husayn (Allaah Amrehemu). Matendo hayo ni mambo ambayo hayakubaliki kisheria na wanachuoni wote wa Kiislam wanapinga na kulaani anayefanya hivyo kwani ni kinyume na mafundisho ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
Amesema Ibn Taymiyyah (Allaah Amrehemu):
"Bid'ah zinazofanyika katika siku hii ni kuwa baadhi ya watu wameitenga na kuifanya kuwa ni siku ya huzuni kwa kuuliwa Al-Husayn (Radhiya Allaahu 'anhu) na kujipiga, kulia wakati Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliharamisha kamailivyo katika Hadiyth hii sahihi:
عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال : قال النبي صلى الله عليه وسلم: ((ليس منا من لطم الخدود وشق الجيوب ودعا بدعوى الجاهلية)) البخاري .
Imetoka kwa Ibn Mas'uud (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema ((Sio miongoni mwetu atakayejipiga mashavuni na kuchanachana nguo na kupiga mayowe ya kijahiliya)) [Al-Bukhaariy]
Na haitoshi hayo wayafanyao, bali wanatukana na kuwalaani Maswahaba wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika siku hiyo."
Ibn Rajab amesema:
"Wanayoyafanya Ma-Rafidhah (Mashia) katika siku hii kuwa ni siku ya huzuni kwa ajili ya kuuliwa Al-Husayn (Radhiya Allaahu 'anhu) ni amali ambazo anazopoteza mtu katika uhai wake akadhani kuwa wanafanya amali njema, wala hakuamrisha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kufanya siku za misiba na vifo vya Mitume kuwa ni siku za huzuni, sasa vipi iwe siku ya huzuni kwa wasio Mitume?"
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atujaalie katika wale ambao husikiliza kauli wakafuata zile zilizo njema. Aamiyn.
Saturday, 26 September 2015
Monday, 7 September 2015
Adhkaar za Jioni
Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee.
Mwenyezi Mungu Mkusudiwa.
Hakuzaa wala hakuzaliwa.
Wala hana anaye fanana naye hata mmoja.
بسم الله الرحمن الرحيم
Kwa Jina La Mwenyezi Mungu Mwingi Wa Rehema Mwenye Kurehemu
Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko,
Na shari ya alivyo viumba,
Na shari ya giza la usiku liingiapo,
Na shari ya wanao pulizia mafundoni,
Na shari ya hasidi anapo husudu.
بسم الله الرحمن الرحيم
Kwa Jina La Mwenyezi Mungu Mwingi Wa Rehema Mwenye Kurehemu
Mfalme wa wanaadamu,
Mungu wa wanaadamu,
Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas,
Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu,
Kutokana na majini na wanaadamu.
ya moto na adhabu ya kaburi”
ajili yako tuko hai na kwa ajili yako tutakufa na ni kwako tu marejeo.
nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unisamehe kwani hasamehe madhambi ila Wewe”
arshi yako na malaika wako, na viumbe vyako vyote kwamba Wewe ndiye Mwenyezi Mungu hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, hali ya kuwa peke yako huna mshirika, na kwamba Muhammad ni mja wako na ni Mtume wako”
(Utasema hivi mara nne)
Atakaye yasema haya asubuhi au jioni mara nne Mwenyezi Mungu سبحانه وتعالى atamuepusha na moto.
اللّهُـمَّ إِنّـي أَعـوذُبِكَ مِنَ الْكُـفر ، وَالفَـقْر ، وَأَعـوذُبِكَ مِنْ عَذابِ القَـبْر ، لا إلهَ إلاّ أَنْـتَ
(mara saba)
(mara tatu )
(mara tatu)
(mara mia moja)
(mara kumi, au mara moja ukisikia uvivu)
(mara mia kwa siku )
(mara tatu)
Saturday, 18 July 2015
Sita Za Shawwaal Na Swawm Nyinginezo Baada Ya Ramadhan
Muhammad Baawazir
Ndugu Waislam, baada ya kuuaga mwezi mtukufu wa Ramadhwaan, ambao umejaa fadhila nyingi na kheri zisizopatikana katika miezi kumi na moja iliyobaki, kuna umuhimu mkubwa wa kuendeleza zoezi hili la Funga baada ya mwezi huu mtukufu hususan, na kwa mwaka mzima kwa ujumla In shaa Allaah.
Swawm kwa ujumla na Swawm za Sunnah haswa ni jambo kubwa sana la ki-'Ibaadah. Na ni bora sana ieleweke ndugu zangu, kuwa Swawm si 'Ibaadah ifanyikayo katika mwezi wa Ramadhwaan pekee, bali ni jambo ambalo linalofanyika mwaka mzima katika nyakati mbalimbali kama tutakavyoona katika makala haya.
Kama ilivyo katika ‘Ibaadah ya Swalah, kuna Swalah za Sunnah au Rawaatib au Nawaafil, ambazo ndizo zitakazokuwa viraka siku ya Qiyaamah wakati zile Swalah za Fardh zitakapopelea katika Mizani. Nazo Swawm za kujitolea au za Sunnah, ndizo zitakazomuongezea mja thawabu na ujira pamoja na ile Swawm yake ya Fardh ambayo ni Ramadhwaan.
Hapa chini tutaziorodhesha Swawm za SUNNAH ambazo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kazipendekeza kwetu tuzitekeleze:
SWAWM YA SIKU SITA ZA MWEZI WA SHAWWAAL
Swawm hii inafuatia moja kwa moja baada ya mwezi wa Ramadhwaan na siku ya 'Iyd ul Fitr. Na Mtume(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
((من صام رمضان ثم أتبعه ستاً من شوال كان كصيام الدهر)) رواه مسلم و الترمذي و ابن ماجه, أبو داود وأحمد
((Atakayefunga mwezi wa Ramadhwaan, kisha akafuatia kwa kufunga siku sita za mwezi wa Shawwaal, basi atapata ujira wa aliyefunga mwaka mzima)).Imepokewa na ma-Imaam Muslim, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Abu Daawuud na Ahmad.
'Ulamaa wanachambua sababu ya kulipwa mja ujira wa mwaka mzima kwa atakayefunga Ramadhwaan na siku sita hizo za Shawwaal, kwa kusema: Jambo zuri hulipwa ujira mara kumi, kwa hiyo mtu akifunga siku 30 za Ramadhwaan atapata ujira mara kumi; nazo zitakuwa 300, ukijumlisha na siku sita za Shawwaal ambazo zikilipwa mara kumi, huwa 60. Kwa hivyo 300 + 60 = 360, mtu atapata hesabu ya mwaka mzima.
Kwa mantiki hii, tunaona kuna umuhimu na ubora mkubwa wa kuifunga Swawm hii ndugu zangu.
SWAWM YA SIKU YA 'ARAFAH (Kwa wale wasio katika Hajj)
Hadiyth ifuatayo inaonyesha uzito na muhimu wa Swawm ya siku hiyo:
عنْ أَبي قتَادةَ رضِي اللَّه عَنْهُ ، قالَ:سئِل رسولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِوسَلَّم: عَنْ صَوْمِ يوْمِ عَرَفَةَ؟ قال:يكفِّرُ السَّنَةَ المَاضِيةَ وَالبَاقِيَةَ رواه مسلمٌ
Imetoka kwa Abu Qataadah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba aliulizwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu Swawm ya 'Arafah akasema ((Inafuta madhambi ya mwaka uliopita na mwaka uliopo)) [Imepokewa na Muslim].
SWAWM YA SIKU TATU KATIKA KILA MWEZI 'AYAAMUL-BIYDHW'
Imesimuliwa na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema:
((من صام ثلاثة أيام من كل شهر فذلك صوم الدهر فأنزل الله عز وجل تصديق ذلك في كتابه {من جاء بالحسنة فله عشر أمثالها} فاليوم بعشرة أيام)) رواه الترمذي قال الشيخ الألباني : صحيح
((Yeyote atakayefunga kila mwezi siku tatu,ni sawa amefunga mwaka mzima, kisha Allaah Akashusha Aayah ithibitishayo maneno ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) isemayo: {{Atakayetenda jambo zuri basi malipo yake ni mara kumi mfano wake}}. Siku moja kwa malipo ya siku kumi))[Imepokewa na At-Tirmidhiy na kasema Shaykh Al-Albaaniy kuwa ni Sahihi].
Ukiitazama Hadiyth hii, utakuta makusudio yaliyotajwa kuwa malipo ya Funga hiyo ya siku tatu za kila mwezi, ni sawa na ya mwaka mzima, ni kuwa, ukipiga hesabu ya hizo siku tatu za kila mwezi, mara miezi kumi na mbili ya mwaka, ni sawa na siku 36. Na siku hizo 36 mara 10 ambazo ndizo malipo ya kila siku kwa mara kumi, basi utapata jumla ya siku 360 ambazo ni takriban idadi ya mwaka mzima wa Kiislam. Fadhila zilizoje na Ujira mrahisi kiasi gani wa kuuchuma ndugu watukufu.
Masiku haya matatu, Masiku Meupe ''Ayaamul-Biydhw'', yametajwa katika Hadiyth ifuatayo:
Abu Dharr Al-Ghifaariy anasimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia:
((يا أبا ذر إذا صمت من الشهر ثلاثة أيام فصم ثلاث عشرة وأربع عشرة وخمس عشرة)) رواهالترمذي. قال الشيخ الألباني: حسن صحيح
((Ee Abu Dharr! Endapo utafunga siku tatu za kila mwezi, basi funga siku ya 13, ya 14, na ya 15)) (Hizi huitwa 'Ayaam ul Biydhw' Masiku Meupe kwa sababu katika masiku hayo kunakuwa kweupe zaidi kwa mwanga wa mbalamwezi). [Imepokewa na At-Tirmidhiy na kasema Shaykh Al-Albaaniy kuwa ni Sahihi].
SWAWM YA JUMATATU NA ALKHAMIYS
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: كان رسول الله صلى الله عليه وسلم يصوم الإثنين والخميس وعندما سئل قال: (( تُعْرَضُ الْأَعْمَالُ يَوْمَ الِاثْنَيْنِ وَالْخَمِيسِ فَأُحِبُّ أَنْ يُعْرَضَ عَمَلِي وَأَنَا صَائِمٌ })) رواه الترمذي وقال حديث حسن
Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) anasimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifunga Jumatatu na Alkhamiys. Alipoulizwa sababu ya Swawm katika siku hizo, akajibu: ((Matendo ya Wanaadam huwekwa mbele ya Allaah kila siku ya Jumatatu na Alkhamiys, nami napenda matendo yangu yawekwe mbele ya Allaah nikiwa nimefunga)). [Imepokewa At-Tirmidhiy na kasema ni Hadiyth Hasan].
SWAWM YA SIKU YA TAASU'AANA 'AASHURAA
Hizi ni Swawm za siku ya tisa na ya kumi ya mwezi wa Muharram (Mwezi wa kwanza katika kalenda ya Kiislam). Hizi ni Swawm kwa kumbukumbu na kumshukuru Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) kwa kumuokoa Nabii Muwsaa (‘Alayhis-Salaam) pamoja na watu wake, kutokana na balaa la Fir’awn na jeshi lake.
SWAWM NYINGINEZO
Swawm katika mwezi wa Muharram zina fadhila nyingi kama Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivyomwelezea Abu Hurayrah. pia Swawm katika mwezi wa Sha'abaan, ambapo mama wa waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) anasema kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikithirisha sana kufunga.
NIYYAH
Swawm kama amali zingine, ni lazima kuwepo na Niyyah ndani yake. Niyyah pahala pake ni moyoni, na si kutamka, ukishapitisha uamuzi wa kufunga, basi hiyo yatosha na si kukariri maneno au kutafuta mtu akufundishe namna ya kuitamka Niyyah kwa Kiarabu au vinginevyo kama wanavyodhania baadhi ya watu.
Wa Allaahu A’lam
Monday, 6 October 2014
Faida za asali
Asali ni chakula kitamu. kinachotengenezwa na nyuki kwa kukusanya nectar kutoka kwenye mauwa.Asali inaweza kaa miaka mingi sana bila kuharibika,asilimi kubwa ya wadudu waaribifu hawawezi kukua ndani ya asali kwani inakiasi kidogo sana cha maji yaani 0.6(WATER ACTIVITY).Tone lolote la maji au mate linapoingia kwenye asali huongeza uwezakano wa kuaribika kwa asali hiyo na kufupisha maisha ya asali.Kwa ufupi naweza sema maji ni adui mkubwa wa asali.
Aina na ubora wa asali hutofautiana kutokana na aina ya nyuki walioitengeneza asali hiyo pomoja na aina ya maua ambayo nyuki wamenyonya nectar yake,rangi za asali pia hutofautiana kwa misingi hiyo hiyo.
Aina mbalimbali za asali.
Apa nchini Tanzania kuna aina kuu mbili za asali,asali ya nyuki wakubwa na asali ya nyuki wadogo.Asali ya nyuki wakubwa hupatikana kwa wingi zaidi kuliko ya nyuko wadogo,Lakini asali ya nyuki wadogo huuzwa bei ghali zaidi ya asali ya nyuki wakubwa kwani ilithibitika kwamba asali ya nyuki wadogo inatengenezwa kutoka kwenye nectar ya mauwa ambayo miti yake inausali wa dawa.Miti hiyo ni kama Mlonge,mwarubaini,rosella na mingine mingi.
Asali ni chakula kinachotumika kwa mambo mengi sana,unaweza itumia badala ya sukari kwenye vinywaji,kuipakaa kwenye mkate,na kuitumia kama kionjo kwenye vyakula mapishi mbali mbali,pia hutumika kutengeneza urembo wa aina mbalimbali kama mafuta na sabuni na vingine vingi,liakini zaidi ya yote asali hutumika kama dawa.
Ni vyema kujua kwamba asali mbichi(ambayo haijapitishwa kwenye moto)ni nzuri kuliko ile iliyopitishwa kwenye moto,Kwani pale asali inapopitishwa kwenye moto baadhi ya enzymes hufa na virutubisho vingine hupotea.Mara nyingi asali hupitishwa kwenye moto ili kuiyeyusha hasa pale inapotakiwa kuchujwa.
ASALI KAMA DAWA
Asali kama dawa inaweza kutibu matatizo mbalimbali,kumbuka tu tunaongelea asali ambayo haijachanganywa na kitu chochote.
For skin rashes, burns and abrasions.
Apply a small amount of raw honey lightly over the affected area; may cover with a dressing or a dusting of cornstarch to reduce any stickiness.
The ultimate moisturizer.
Smooth a small amount of raw honey lightly over the skin; easily remove later with splashes of cold water or comfortable warm water. Leaves skin baby soft.
As a bath and antibacterial soap.
Wash with raw honey straight from the jar and enjoy sparkling clean skin. Facial blemishes and acne caused by cosmetics or allergies will clear up quickly using a nightly treatment of RRH. A small amount needed.
For hair and scalp treatment.
Apply Really Raw Honey (with or without olive oil) to dry or damp hair about one half hour before washing–you’ll be amazed at your “crowning glory”.
For dental care and mouth sores.
Cleans teeth, mouth and dentures and stops bleeding gums. Canker sores, blisters and mouth ulcers respond to application of raw honey.
An astounding natural preservative.
Unprocessed honey found in ancient tombs was determined to be edible and was even used to preserve bodies. Keeps foods fresh and moist longer and retards spoilage.
For healing ulcers and burns
Also many years ago, a study by Robert Bloomfield, published in the Journal of the American Medical Association, reports “Applied every 2 to 3 days under a dry dressing, honey promotes healing of ulcers and burns better than any other local application. It can also be applied to other surface wounds, including cuts and abrasions…”
Honey has anti-cancer properties.
Recent studies by Gribel and Pashinskii indicated that honey possessed moderate antitumor and pronounced anti-metastatic effects in five different strains of rat and mouse tumors. Furthermore, honey potentiated the antitumor activity of chemotherapeutic drugs such as 5-fluorouracil and cyclophosphamide. — Gribel, N.V., and Pashinskii, V.G. Antitumor properties of honey. Vopr. Onkol., 36:704-709, 1990.
C.V. Rao at the American Health Foundation in Valhalla, New York found caffeic acids in propolis are inhibitors of colon cancers in animals. Other research shows hive products have the ability to prevent and halt the spread of malignant diseases. Earlier research by M.T. Huang also published in Cancer Research found caffeic acids effective in inhibiting skin cancer tumors in mice.
Ushauri
Ni vyema ukawa na asali nyumbani kwa ajili ya matumizimbalimbali.Kwa matumizi ya asali kama dawa,nashauri asali mbichi ya nyuki wadogo.Najua ni ngumu kujua kama asali mbichi au imepitishwa kwenye moto,Hivyo nashauri utumie asali ya FANO 2010.
Asali za Fano 2010(Golden Lulu)
Asali za FANO 2010 zinapatika Thanks God supermarket,eneo la sinza madukani.nashauri asali hii kwani ndio asali ninayotumia na ninakuhakikishia kuwa ni asali mbichi,na zaidi ya yote niliwai tembelea workshop ya FANO 2010 na kuona jinsi wanavyochuja asali ,Ndio maana ninanguvu ya kushauri utumie asali hio
ONYO
Asali si nzuri kwa watoto wadogo wenye umri wa kati ya siku moja hadi miaka miwili,kwani wakati mwingine asali huwa na endospores wa bacterium clostridium botulinum.Endospores hizo zinaweza kubadilika kua aina ya bacteria wanatoa sumu.Bacteria hawa hushambulia utumbo mwembamba wa mtoto ambao haujakomaa na hivyo huweza msababishia mtoto kuumwa na hata kifo.
Akina mama msikose chupa ya asali jikoni,kwani ajali za kuungua ni kawaida jikoni na asali ni dawa nzuri sana,Ukiungua kitu cha kwanza kabisa pakaa asali nyingi kwenye eneo uliloungua..
Nimalizie kwa kusema.Asali ikichanganywa na dawa zingine za asili au viungo fulani pia huwa dawa ya magojwa mengi zaidi.Naamini makala hii imekufumbua macho na kukufanya uithamini asali
Friday, 26 September 2014
Uzushi Wa Unoadaiwa Ni Fadhila Za Siku Kumi Za Dhul-Hijjah
SWALI:
Nimepokea e-mail iliyotumwa yenye kutaja fadhila za siku kumi kila siku kuwa ni jambo fulani limetokea na kadha kama inavyoeleza hapa chini. Je hii ipo dalili au ni katika uzushi?
Siku Kumi Bora
Mwenye-ezi mungu subhanahu wataala ameapa kwa masiku bora katika quraan takatifu sura 89 aya 1-2 isemayo : Mtume Muhammad ( S.A.W.) ametusimulia vilivyotendeka na umuhimu wa siku hizi kumi bora za mfungo tatu (DhulHijja); Rasula-llah atueleza sisi ummati wake kuwa, mwenye kufunga siku hizo hupata fadhla kubwa mno,kwani kila siku ina fadhila na kheri zake:
SIKU YA KWANZA YA MFUNGO TATU Mtume (S.A.W.) asema kuwa - "Ni siku ambayo Mwenye-ezi Mungu alimsamehe Nabii Adam (A.S.) kwa makosa yake".Mwenye kufunga siku hiyo, Mwenye-ezi Mungu humsamehe madhambi yake.
SIKU YA PILI YA MFUNGO TATUMtume(S.A.W.)asema kuwa:-"Ni siku ambayo Mwenye-ezi Mungu alikubali maombi ya Nabii Yunus (A.S.) ya kumtoa katika matumbo ya samaki".Mwenye kufunga siku hiyo, ni kama aliyefanya ibada ya mwaka mzima pasi na kufanya makosa.
SIKU YA TATA MFUNGO TATU Mtume(S.A.W.)asema kuwa:-"Ni siku ambayo Mwenye-ezi Mungu aliitikia Dua ya Nabii Zakariya (A.S.) yakumpata mtoto".Mwenye kufunga siku hiyo, Mwenye-ezi Mungu huitikia dua yake.
SIKU YA NNE YA MFUNGO TATUMtume(S.A.W.)asema kuwa:-"Ni siku ambayo alizaliwa Nabii Issa(A.S.)".Mwenye kufunga siku hiyo, Mwenye-ezi Mungu humuondolea matatizo na umasikini.
SIKU YA TANO MFUNGO TATU Mtume(S.A.W.)asema kuwa:-"Ni siku alizaliwa Nabii Musa(A.S) "Mwenye kufunga siku hiyo, Mwenye-ezi Mungu humtakasa na unafiki na humuondolea adhabu za kabori.
SIKU YA SITA MFUNGO TATU Mtume (S.A.W.)asema kuwa:-Ni siku ambayo Mwenye-ezi Mungu alimfungulia Mtume wake (Muhammed (S.A.W.) )kheri".Mwenye kufunga siko hiyo, Mwenye-ezi Mungu humuangalia kwa jicho la huruma wala hapati adhabu siku ya kiyama.
SIKU YA SABA YA MFUNGO TATU Mtume asema kuwa:-"Ni siku ambayo Milango ya Jahannam(Moto)hufungwa na hayafunguliwi hadi masiku kumi yatimie".Mwenye kufunga Mwenye-ezi Mungu humfungia Milango thelathini ya mambo mazito na humfungulia Milango thelathini ya mambo mepesi.
SIKU YA NANE YA MFUNGO TATUMtume(S.A.W.)asema kuwa:-"Ni siku iitwayo Tar-wiya".Mwenye kufunga hupewa malipo ambayo hakuna ayajuwaye isipokuwa Allah SWT.
SIKU YA TISA YA MFUNGO TATUMtume(S.A.W.)asema kuwa:-"Ni siku iitwayo Arafat".Mwenye kufunga siku hiyo, hufutiwa makosa ya mwaka uliopita, na utakao kuja.
SIKU YA KUMI YA MFUNGO TATU:- Mtume(S.A.W.)asema kuwa:-"Ni siku ya kuchinja Mnyama(itakuwa Iddi Kubwa), tone la kwanza la damu litakapo tona Mwenye-ezi Mungu humsamehe dhambi zake na za jamaa zake. Na mwenye kumpa chakula Masikini au akatowa sadaka siku hiyo, Myenye-ezi Mungu atamfufua siku ya Kiyama kwa amali na mizani ya uzito, thawabu zake zitashinda uzito wa Mlima Uhud".
PLEASE DO NOT FORGET TO ENLIGHTEN OTHER MUSLIMS BY FORWARDING THIS MAIL
JIBU Kutoka alhidayah
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wasallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho
Tunasikitika kwamba siku hizi fitna za kusambaza uzushi zimezidi kutokana na wepesi wa mawasiliano kupitia barua pepe (e-mail), simu za mkononi n.k. Jambo linaloshangaza ni kwamba Hadiyth zilizo Sahihi zimejaa tele lakini hizo hazisambazwi kama zinavyosambazwa za uzushi. Ni dhahiri kwamba wanaofanya hivyo ima hawajui tofauti ya mafunzo sahihi na yale potofu ima kwa uchache wa elimu, au kwa pupa tu za kutafuta thawabu kwa njia za mkato ndiko kunakowasababisha wao kueneza haya mambo yasiyo na dalili wala asili. Lakini wanaghafilika ndugu hao kutambua madhara yanayopatikana kutokana na hayo wanayoyaeneza kila mara.
Moja ya madhara makuu ni kupoteza mafundisho sahihi ya Dini yetu, na kueneza ya uongo na hivyo kutawala upotofu katika jamii ya Kiislam, Kwani kama wanavyosema wema waliotangulia, kuwa, bid’ah inavyoenea, ndio Sunnah hupotea.
Tumepekuwa vitabu mbalimbali vya Hadiyth vikubwa na mashuhuri na hakuna hata sehemu moja tuliyokuta kuna Hadiyth inayotaja Fadhila za masiku kumi ya Dhul-Hijjah kwa mtindo huo na kwa maelezo hayo! Vilevile Maulamaa waliowahi kukumbana na maelezo hayo, wamesema kuwa ni ‘Mawdhuw’ – yaani ya kutungwa na si ya kweli.
Kuna hatari vilevile ya watu kutumbukia katika maonyo na makemeo aliyoyatoa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((من كذب علي متعمدا فليتبوأ مقعده من النار)) متفق عليه
((Atakayeniongopea makusudi basi ajitayarishie makazi yake motoni)) [Al-Bukhaariy Na Muslim]
Ukiwa umeeneza mambo hayo na hali unajua kuwa si sahihi, basi tambua kuwa ushaingia katika walioelezwa ndani ya Hadiyth hiyo.
Na ikiwa una mazoea ya kueneza au kutuma kila unachopata ukidhani utapata thawabu kwa kufanya hivyo na hali huna uhakika nacho, au huna elimu ya jambo hilo kama ni sahihi au la, basi utakuwa pia una majukumu kwa kuwa Uislam umesisitiza sana elimu na umuhimu wa kuitafuta; hivyo kwanini ubakie katika ujinga na kutokufahamu unayotuma? Pia ikiwa hujui, ushaelezwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) uulize wenye elimu na upambuzi, je, ulijaribu kufanya hayo kabla hujasambaza mambo hayo ya kutunga yenye kupotezea Waislam muda, juhudi, na hata ‘amali zao kwa kufanya yasiyo sahihi na yasiyo katika mafundisho ya Dini?
Na madhara mengine ni kwamba dhambi za mwenye kueneza uzushi huzidi kila uzushi unapozidi kusambaa na mwenye kuanza kueneza uzushi hubeba dhambi za kila mtu anayepokea na kujifunza uzushi huo:
عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال : ( من دعا إلى هدى كان له من الأجر من أجور من تبعه لا ينقص من أجورهم شيئاً ومن دعا إلى ضلالة كان عليه من الإثم مثل آثام من تبعه لا ينقص ذلك من آثامهم شيئاً) رواه مسلم
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: ((Atakayelingania kwenye uongofu atapata thawabu (ujira) wa yule atakayemfuata bila ya kupungukiwa chochote katika thawabu zao. Na atakayeelekeza katika upotofu atapata dhambi mfano wa dhambi za yule atakayefuata bila ya kupungukiwa chochote katika dhambi zao)) [Muslim]
Tumefanya utafiti mkubwa kutafuta kauli kama hizo kuhakikisha kama ipo kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inayotaja fadhila za siku hizo kama zilivyotajwa humu lakini hatukupata. Mojawapo ya matokeo ya utafiti ni kupata fatwa kutoka kwa Maulamaa kutoka Markaz ya Fataawa walioulizwa kuhusu ujumbe huo nao pia wamehakikisha kuwa ni uzushi usio na dalili yoyote [Markaz al-Fataawa 24 Dhul-Hijjah 1424/16-02-2004].
Tunawanasihi ndugu zetu Waislamu wasome mada muhimu katika kiungo kifuatacho ili watambue hatari ya kueneza uzushi:
Hatari Ya Kueneza Hadiyth Dhaifu Na Visa Vya Uongo
Vilevile mtu anatakiwa asome mada hii hapa chini yenye kuhusu uzushi wenye kufanana na huo:
Uzushi Unaodaiwa Kuhusu Mambo Yaliyotokea Siku Ya Ashuraa Tarehe 10
Jambo jingine muhimu tunalopenda kuwatanabahisha ni kuhusu jinsi hayo majina ya miezi ya Kiislam yanavyoitwa au yalivyozoeleka kuitwa kama tulivyoona kwenye huo ujumbe wa kutungwa kwa jina la mfungo mosi, mfungo pili, mfungo tatu n.k., hakika ni majina yaliyozoeleka lakini si sahihi kwani yanapoteza ufahamu wa majina sahihi na mpangilio wa hiyo miezi ya Kiislam.
Miezi ya Kiislam hujulikana mwezi wa kwanza kama ni Muharram lakini wao huo mwezi wa kwanza umeitwa ni mfungo nne, na mwezi wa Dhul-Hijjah ambao ni mwezi wa kumi na mbili, wao wanauita mfungo tatu! Hivyo Waislam wengi hudhani kuwa huu mwezi wa 12 wa Dhul-Hijjah tulionao sasa kuwa ni mwezi wa 3 badala ya 12. Kutoka katika mpango uliowekwa na Uislam na kufuata mipango na taratibu za kimila na kitamaduni, kunasababisha mafunzo ya Dini kutofahamika kamwe, au kusahaulika kabisa. Leo hii, Waislamu wengi Waswahili hawajui miezi ya Kiislam kwa majina yake ingawa wengi wanaijua hiyo ‘mifungo’. Huo ni ukweli wenye kusikitisha. Na wengi huita kalenda na tarehe za Kiislam kuwa ni tarehe za Kiarabu badala ya Kiislam; ilihali kuna tofauti kubwa kati ya Uislamu na Uarabu. Miezi ya Kiislam ni hiyo tuliyozungumzia hapo juu na tutaweka chini kabisa mpangilio wake wa majina ya miezi yote ya mwaka mzima. Kalenda au tarehe za kiarabu ni tofauti na za Kiislam na mtu akitaka kujua atazame magazeti ya Kiarabu ataona tofauti. Hivyo, Waislam wajizoeshe kuita tarehe za Kiislam au miezi ya Kiislam na si ya Kiarabu, maana kuna Wakristo Waarabu nao hawafuati kalenda yetu ya Kiislam.
Miezi Ya Kiislam (Kila Muislam Ajitahidi Kuijua Na Kuihifadhi)
1- Muharram محرّم
2- Swafar صفر
3- Rabiy’u al-Awwal ربيع الأول
4- Rabiy’u ath-Thaaniy au Rabiy’u al-Aakhirربيع الآخر أو ربيع الثاني
5- Jumaada al-Uwlaa جمادى الأول
6- Jumaada ath-Thaaniy au Jumaada al-Aakhir جمادى الآخر أو جمادى الثاني
7- Rajab رجب
8- Sha’abaan شعبان
9- Ramadhaan رمضان
10- Shawwaal شوّال
11- Dhul-Qa’adah ذوالقعدة
12- Dhul-Hijjah ذوالحجة
Inasikitisha sana kuona Muislam
kahifadhi miezi yote ya kikafiri, lakini hawezi kutaja hata miezi sita ya Kiislam. Sana sana utakuta Muislam anajua ile miezi ya karibu na Ramadhaan kama Rajab, Sha’abaan na pia labda mwezi huu wa Dhul-Hijjah na wengine huujua Rabiy’ul al-Awwal kwa sababu ya kusherekea tu Mawlid na huenda asijue kuwa ni Rabiy’u al-Awwal, bali atakuwa anaujua kwa jina la kijamii ‘Mfungo sita’! Huu ndio msiba tulionao Waislam, inatubidi tuamke hivi sasa na tuzindukane na usingizi wa miaka na miaka. Na silaha pekee ya kuzindukana na hayo, ni ELIMU SAHIHI ya Dini.
Pia tunawaomba ndugu zetu kwamba wanapopata jambo lenye shaka kwanza wawe wanahakikisha kabla ya kutuma kwa wenzao kwani tutambue kuwa Muislamu inapomfikia kauli inayodaiwa kuwa ni ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) basi imeshakuwa ni waajib kwake kuhakikisha. Akipata dalili ya usahihi wake atume kwa wenziwe kama tunavyoamrishwa kufikisha kwa wengine japo Aayah moja na kuamrishana mema na kukatazana maovu. Lakini ikiwa hakupata dalili yake ni bora kuacha kutuma kuliko kuleta madhara ya uzushi na kuzidisha ufisadi katika dini na jamii kwa ujumla kwa kupoteza mafunzo sahihi na kueneza mafunzo ya uzushi.
Kidokezo Cha Kuweza Kutambua Hadiyth Zisizo Sahihi Au Ujumbe Wa Uongo:
Ndugu Muislam, ukitaka kugundua haraka ujumbe ulioupata kwenye barua pepe (e-mail) au ujumbe kwenye simu za mkono, kwanza kitakachokujulisha kuwa ujumbe huo una utata na sio sahihi, ni kuwa, mara nyingi maelezo yaliyomo ndani ya ujumbe huo zikiwemo zinazosemwa ni Hadiyth, utakuta hazitajwi zilipotolewa, kama ni Hadiyth utaona haisemwi nani kasimulia, nani kapokea, kitabu gani, hakuna hata Imaam wa Hadiyth (Muhaddith) aliyetajwa kwenye Hadiyth hiyo n.k. Hayo yote yanatosha kumtia mashaka mtu kuhusiana na alichokipokea. Hivyo, endapo utapokea ujumbe au Hadiyth ambayo imekuja tu na kudaiwa kasema Mtume, bila kutajwa zaidi ya hivyo… basi mrudishie aliyekutumia na muombe akueleze Hadiyth hiyo iko kwenye kitabu kipi, na nani kaisimulia na kama ni sahihi au dhaifu. Usiwe na pupa ya kueneza au kusambaza kwa wengine hadi kwanza upate uhakika 100%. Vilevile unaweza kutuandikia maswali@alhidaaya.comkuulizia masuala kama hayo na inshaAllaah tutakusaidia haraka katika masuala hayo.
Na Allaah Anajua zaidi